Matapeli wa meseji za simu wawashiwa moto
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kupitia kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandaoni, (Cybercrime investigation unit) kimesema kuwa kinafanya uchunguzi kuwabaini wanaotuma ujumbe mfupi wa simu za mkononi kwa nia ya kuwatapeli wananchi.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, Makao makuu, Barnabas Mwakalukwa, leo imesema yeyote aliyetapeliwa anatakiwa kutoa taarifa katika kituo cha polisi alichokaribu nacho.
“Tunawataka wananchi kuacha kutumia simu na mitandao ya kijamii vibaya na badala yake itumike kuhabarisha na kuelimisha jamii juu ya mambo mbalimbali ya maendeleo,” imesema taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesema, baadhi ya jumbe hizo ni zile zinazosema. ‘Ile hela tuma kwa namba hii’ au ‘usipige kwa sasa, spika imeharibika, tuma ujumbe,’ au ‘Mjukuu wangu ile ndagu niliyokutumia imefanya kazi na sasa unapata wateja wengi... sasa njoo uchukue ndagu nyingine ya mvuto na nyingine kama hizo.’
Mfano wa meseji za matapeli
Pamoja na hayo Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kutumia mitandao pamoja na simu katika kulimisha na kuhabarisha na si vinginevyo ikiwa ni pamoja na kuwataka wananchi kupuuzia jumbe hizo zenye lengo la kitapeli.
Ruby akiimba SHOW mbele ya maelfu ya watu
Post a Comment