Kombe la Dunia 2018: Makundi yalivyo na ratiba ya mechi
Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaendelea nchini Urusi.
Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.
Fainali itachezwa 15 Julai.
Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.
Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.
Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962.
Hapa ni mwongozo wa makundi yalivyo na mechi zitakavyochezwa hatua ya makundi:
Brazil wanatafuta kuweka rekodi nyingine kwa kushinda kombe hilo kwa mara ya sita.
Michuano hiyo ya mwezi mmoja inatarajiwa kuwavutia mashabiki nusu milioni kwenda Urusi na kote duniani inatarajiwa kutazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu.
Kuna makundi manane, kila kundi likiwa na timu nne.
Timu mbili ambazo zitamaliza juu kwenye kundi ndizo zitakazosonga hadi hatua ya 16 bora.
Fainali itachezewa katika uwanja wa Luzhniki ambao hutoshea mashabiki 81,000 mnamo 15 Julai.
Nani atashinda Kombe la Dunia?
Mabingwa watetezi Ujerumani, mabingwa mara tano Brazil, washindi wa Euro 2016 Ureno, waliomaliza wa pili 2014 Argentina, Ubelgiji, Poland na washindi wa mwaka 1998 Ufaransa ni timu nane ambazo zilikuwa kwenye chungu wakati wa kufanywa kwa droo.
Wote wanapigiwa upatu kushinda.
Unaweza kusoma pia:
Mike Kalambay Belela
Post a Comment