Watu watatu watiwa mbaroni kwa tuhuma za kuwaua Simba tisa
Maafisa nchini Tanzania wanasema wamewatia mbaroni watu watatu wanoshukiwa kuwapatia sumu simba tisa katika mbuga maarufu ya taifa hilo ya Serengeti.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema, maafisa wa mbuga hiyo waligundua mizoga ya simba hao wikiendi iliyopita.
Simba saba waliuawa katika tukio lingine kama hilo, katika mbuga hiyo hiyo mwaka wa elfu mbili na kumi na tano.
Katika nchi jirani ya Uganda, simba kumi na moja walipatikana wamekufa katika tukio linaloshukiwa kuwa ni la sumu katika mbuga ya wanyama ya Queen Elizabeth.
Msemaji wa Hifadhi ya Taifa Pascal Shelutete amsema kwamba waligundua vifo vya simba hao baada ya kula mizoga ya ngo'mbe waliokuwa wakifugwa kandokando ya hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Namna na sababu ya kupewa sumu hiyo bado haijawekwa wazi lakini Shelutete anasema uchunguzi bado unaendelea.
Baada ya simba hao kufa, watuhumiwa wa tukio hilo wanadaiwa kukata mikia na miguu yao na kuondoka nayo, jambo ambalo kwa mujibu wa polisi linadaiwa kuongeza walakini juu ya tukio hilo.
Mwaka wa 2015, simba saba waliuawa kwa namna hiyo hiyo huku 2017 simba wengine watatu walipigwa risasi na kufa katika kambi hiyo.
Mwezi April katika nchi jirani ya Uganda , simba 11 walikutwa wamekufa kwa kupewa sumu katika Hifadhi ya Taifa ya Malkia Elizabeth.
Polisi mkoani Mara Kaskazini Magharibi mwa Tanzania inasema watuhumiwa watatu waliokamatwa watafikishwa mahakamani baada tu ya upelelezi kukamilika.
Mbuga ya wanyama ya serengeti ndio kongwe na kubwa zaidi nchini Tanzania ikiwa na kilomita zaidi ya elfu 14 huku kwa mwaka ikikadiriwa kuwa na watembeleaji zaidi ya laki tatu na 50.
Dr SHIKA Afanikiwa Kuingiza Mabilioni Yake Tanzania Leo...Tazama Hii
Post a Comment