Wanaume waundiwa njia mpya kupimwa VVU
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajia kuzindua rasmi kampeni ya kitaifa ya upimaji virusi vya Ukimwi VVU iliyopewa jina la ‘Furaha Yangu’ yenye lengo la kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema hasa kwa wanaume.
Kampeni hiyo itakayozinduliwa Juni 19 mwaka huu mjini Dodoma, inalenga kuwaleta wanaume kwenye huduma kutokana na wengi wao kuwa waoga kuzifikia.
Akizungumza Kaimu Mkurugenzi Kinga kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Angela Ramadhani amesema kampeni hiyo inahamasisha mkakati mpya wa Serikali wa upimaji wa VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na VVU.
“Katika dira ya kuwa na taifa bila Ukimwi, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90 ambapo asilimia 90 ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU, asilimia 90 ya wenye maambukizi kuanza dawa na asilimia 90 ya walioanza dawa kupunguza kiwango cha VVU mwilini,” amesema Dkt Angela.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk Laonald Maboko amesema kampeni hiyo ni matokeo ya utafiti wa awali wa nne uliofanywa na Taasisi ya Takwimu nchini NBS, ambao ulionyesha pamoja na mambo mengine hamasa miongoni mwa wananchi na hasa wanaume katika kuziendea huduma za upimaji wa VVU nchini ni ya kiwango cha chini.
MTOTO ATOA SIRI YA LIYO MKUTA
Post a Comment