Ajinyonga kwa kukataliwa tendo la ndoa
Mwanaume mmoja Nchini Uganda aliyetambulika kwa majina Joseph Ojur mwenye miaka 52 mkazi wa ukanda wa Kabagu katika manispaa ya Njeru amejinyonga mpaka kufa baada ya kunyimwa ‘unyumba’ na mkewe.
Kamanda wa Polisi eneo la Njeru, Christopher Tuhunde amesema kuwa, marehemu alijinyonga ndani ya nyumba yake na jeshi hilo linaendelea kuchunguza kwa undani juu ya tukio hilo ili kuja na ripoti kamili kuhusiana na kujinyonga kwa Ojur.
“Naomba niwashauri ndugu zangu kuwa muwazi na penda kuomba ushauri kwa majirani juu ya matatizo yanayowakabili kuliko kukimbilia kujiua”, amesema Kamanda Tuhunde
Taarifa za awali zinasema kuwa mwanaume huyo alifanya vipimo vya afya yake na kugundua kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ndipo mkewe alianza kumkatalia kufanya naye tendo la ndoa.
NILIANGUKA NA UNGO WA KICHAWI KANISANI
Post a Comment