Rais atangaza zoezi la ukaguzi wafanyakazi
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa serikali yake iliyopo madarakani itafanya zoezi la ukaguzi wa aina ya maisha wanayoishi wafanyakazi wa umma.
Rais Kenyatta amesema wafanyakazi wote wa umma akiwemo yeye mwenyewe na Naibu wake William Ruto watatakiwa kutoa maelezo ya mali wanazomiliki na wale watakaobainika kuiba fedha za umma watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.
Kauli ya Rais Kenyatta ameitoa wakati huu ambapo nchi hiyo ikishuhudia kampeni kubwa ya kupambana na vitendo vya rushwa ambapo hivi karibuni maofisa kadhaa wa serikali walikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya ubadhirifu wa mali za umma na matumizi mabaya ya ofisi.
Maafisa wa serikali na watu wengine zaidi ya 40 wameshtakiwa kwa wizi wa mamilioni ya Dola zilizokuwa zimetengewa kwa ajili Shirika la Huduma kwa Vijana NYS.
Post a Comment