Header Ads

Thomas Lemar: Atletico Madrid wamchukua mchezaji aliyekuwa anatafutwa na Wenger

Thomas Lemar
Atletico Madrid wameafikiana "makubaliano ya awali" ya kumchukua winga wa Monaco Thomas Lemar ambaye alikuwa akitafutwa sana na Arsenal kabla ya kuondoka kwa Arsene Wenger.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa - ambaye amekaa misimu mitatu tangu kuwasili Monaco akitokea Caen, kwa sasa yupo Urusi kucheza michuano ya Kombe la Dunia.
Arsenal walishindwa kumnunua Lemar, 22, kipindi cha kuhama wachezaji majira ya joto mwaka jana.
Alikuwa pia akitafutwa na Liverpool waliotaka kulipa £60m.
"Katika siku zinazofuata, klabu hizi mbili sasa zitafanya juhudi kukamilisha uhamisho huo," Atletico wamesema.
Lemar amefunga mabao 22 katika mechi 123 alizochezea Monaco na aliwasaidia kushinda Ligue 1 na kufika nusufainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu wa 2016-17.
Alichezea timu ya taifa ya Ufaransa mara ya kwanza 2016 na amewafungia mabao matatu katika mechi 12 alizowachezea tangu wakati huo.
Kikosi kamili cha Ufaransa Kombe la Dunia:
Walinda LangoHugo Lloris (Tottenham Hotspur), Steve Mandanda (Marseille), Alphonse Areola (Paris Saint-Germain)
WalinziLucas Hernandez (Atletico Madrid), Presnel Kimpembe (Paris Saint-Germain), Benjamin Mendy (Manchester City), Benjamin Pavard (Stuttgart), Adil Rami (Marseille), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona), Raphael Varane (Real Madrid)
Viungo wa katiN'Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (Juventus), Steven N'Zonzi (Sevilla), Paul Pogba (Manchester United), Corentin Tolisso (Bayern Munich)
WashambuliajiOusmane Dembele (Barcelona), Nabil Fekir (Lyon), Olivier Giroud (Chelsea), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Thomas Lemar (Monaco), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Florian Thauvin (Marseille)

No comments