Volkano yasabisha vifo vya watu saba
Serikali ya Guatemala imesema kuwa majivu ya volkano kutoka mlima mmoja unaoendelea kulipuka, yamesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine ishirini.
Shirika la kukabiliana na majanga nchini Guatemala limesema kuwa mlima Fuego ulilipuka siku ya jumapili, huku majivu hayo yakirushwa hadi kijiji cha El Rodeo na kusababisha uharibifu mkubwa wa makaazi ya watu. Baadhi yao waliteketea ndani ya nyumba hizo.
Rais wa taifa hilo Jimmy Morales amesema vikosi vya uokoaji vimeanza kazi na tahadhali imetolewa.
Hata hivyo ya watu hao waliokufa kati yao watatu ni watoto.Mlipuko wa Volcano hii unatajwa kuwa Zaidi tangu ule uliotokea mwaka 1974.
Serikali ya Guatemala inasema kuwa takribani watu milioni moja wameathirika kutokana na Volcano hiyo.
Hata hivyo ushauri umetolewa kwa raia kuvaa vifaa vya kuzuia pua zao kutokana na moshi na majivu yanayoendelea kurushwa kutokana na Volcano hiyo.
Dr SHIKA Afanikiwa Kuingiza Mabilioni Yake Tanzania Leo...Tazama Hii
Post a Comment