Ujumbe wa Rais Magufuli kufuatia vifo vya mapacha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na Watanzania kuomboleza msiba wa watoto Maria na Consolata, waliofariki dunia hapo jana hospitalini mkoani Iringa.
Kwenye ukurasa wa twitter Rais Magufuli ametuma ujumbe akielezea kusikitishwa kwake na msiba wa watoto hao, ambao alishawahi kuwatembelea walipokuwa hospitali ya Muhimbili wakipatiwa matibabu hivi karibuni.
“Nimesikitishwa na kifo cha Maria na Consolata. Nilipokwenda hospitali waliliombea Taifa. Walikuwa na ndoto ya kulitumikia Taifa. Poleni familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa, pumzikeni mahali pema wanangu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe”, ameandika Rais Magufuli kwenye ukurasa wake wa twitter.
Watoto Maria na Consolata ambao waliungana mwili wamefariki dunia wakipatiwa matibabu hospitali ya mkoa Iringa, siku chache baada ya kuruhusiwa kutoka Hospotali ya Taifa Muhimbili, ambako walikuwapo zaidi ya miezi miwili wakipatiwa matibabu.
Taarifa kutoka Hospitali mkoani Iringa zinasema kwamba watoto hao walifariki kwa muda tofauti, ambapo mmoja alifariki saa Dr SHIKA Afanikiwa Kuingiza Mabilioni Yake Tanzania
Leo...Tazama Hii1 usiku, na mwengine alifariki saa 3 usiku.
Post a Comment