JENEZA LITAKALOBEBA MIILI YA MAREHEMU MARIA NA CONSOLATA
Hili ndilo sanduku/jeneza litakalobeba miili ya wapendwa wetu Marehemu Maria na Consolata likiwa tayari limekamilika kwa maziko hapo kesho Jumatano Juni 6,2018 katika makaburi ya masista na mapadre pamoja na viongozi wa kanisa Katoliki, Tosamaganga mkoani Iringa
Maria na Consolata wanazikwa kesho baada ya ukamilisho wa ibada ya kuwaaga itakayofanyika kwenye viwanja vya Rucu kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Tosamaganga watakakozikwa.
Maria na Consolata wanazungukwa na makaburi ya masista waliokwishafariki.Maria na Consolata walifariki dunia June 2 mwaka huu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ambapo walikuwa wakipatiwa matibabu.
Post a Comment