Sababu za mapacha kuungana
Imeelezwa kuwa hali ya watoto kuungana hutokea wakati wa mgawanyiko wa seli ingawa
si mara zote na chanzo kikuu ni makosa ya taarifa za vinasaba katika mfumo wa uzazi.
Hayo yameelezwa na Dk. Festo Dugange wakati akizungumza na eatv.tv katika mahojiano maalum ambapo amesema kuwa makosa ya taarifa za ‘DNA’ hushindwa kugawanya yai na ndipo hutokea mapacha hao.
"Mbegu ya baba ikikutana na yai la mama ili kutengeneza mtoto, huwa kunatokea mgawanyiko wa seli mara 18 sasa iwapo seli hizo hazikugawanyika na kuachana ikiwa mimba hiyo ni ya watoto pacha basi huzaliwa wakiwa wameungana baadhi ya viungo vyao,” amesema Dk. Dugange.
Ameongeza kuwa hali hiyo inapotokea wakati mwingine mtoto mmoja hukutwa akiwa amekamilika viungo vyote huku mwenzake akiwa na kasoro kadhaa.
NILIANGUKA NA UNGO WA KICHAWI KANISANI
Post a Comment