Baraza la Shirikisho la Soka Duniani
(FIFA) limeidhinisha uamuzi wa kulipatia bara la Afrika nafasi tisa
timu zinazoshiriki fainali za Kombe la Dunia zitakapoongezwa na kuwa 48
mwaka 2026.
Hatua hiyo iliidhinishwa Jumatano nchini Bahrain. Bara la Afrika kwa sasa huwa na nafasi tano pekee.
Taifa
la kumi kutoka Afrika litashiriki katika michuano ya muondoano ya
kufuzu, itakayoshirikisha nchi sita, kuamua atakayefaidi kutokana na
nafasi mbili za ziada. Baraza la Fifa lilitangaza pendekezo lake la kwanza kuhusu mpango wa kugawa nafasi hizo 48 tarehe 30 Machi. Nafasi mpya zitajazwa vipi? Afrika - 9 kutoka timu za awali 5 Asia - 8 kutoka timu 4 za awali Ulaya - 16 kutoka timu 13 za awali Marekani ya Kaskazini, Kati na Caribbean - 6 kutoka timu 4 za awali Bara la Oceania - 1 kutoka timu 1 ya awali Amerika ya Kaskazini - 6 kutoka timu 4 za awali Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia
Post a Comment