Mtandao wa kijamii wa Facebook bado unatumika nchini Thailand, licha ya muda wa mwisho kukamilika
Mtandao wa kijamii
wa Facebook bado unatumika nchini Thailand, licha ya muda wa mwisho
kukamilika wa kuitaka Facebook, kuondoa taarifa ambazo utawala wa nchi
hiyo umezitaka kuwa potovu kwake.
Facebook ilikuwa imepewa muda
wa hadi 10:00 (04:00 GMT) kuondoa kurasa 131 ambazo Thailand ilisema
zinakiuka sheria zake kali za lese-majeste
Zaidi ya watu 100 wamefunguliwa mashtaka chini ya sheria hiyo tangu yafanyike mapinduzi ya kijeshi miaka mitatu iliyopita.
Utawala ulitishia kuchukua hatua za kisheria na kuufunga kabisa mtandao wa Facebook.
Baada ya muda uliotangazwa kupita katibu katika kampuni
inayosimamia mawasiliano nchini Thailanda, aliwaambia waandishi wa
habari kuwa amri za mahakama zimetolewa kwa kurasa 34, na utawala huo
ulikuwa ukitafuta amri zingine kwa kusara zingine 97.
Wathailand ni kati ya watumiaji wakubwa zaidi wa
Facebook barani Asia, huku maelfu ya biashara ndogo zikiutegemea mtandao
huo kama chomo kikuu cha mauzo.
Ikiwa serikali itatekeleza
vitisho vyake na kuwalazimisha watoa huduma za mitandao kuifunga,
kutakuwa na malalamiko makubwa nchini humo.
Hata
hivyo serikali ina matumaini ya kuhakikisha kuwa hakuna taarifa
zinazotajwa kuwa mbaya, zitaruhusiwa kuonekana nchini Thailand licha ya
kuwepo changamoto z
Post a Comment