Header Ads

wajua kifua kikuu kina uwa



Kifua Kikuu (Tuberculosis) ni ugonjwa wa kuambukiza, ambao mara nyingi hushambulia mapafu. Ugonjwa huu unachukua nafasi ya pili ya magonjwa yanayosababisha vifo duniani.
Mwaka 2015, watu wapatao milioni 1.8 wanakadiriwa kufa kwa ugonjwa huu, huku idadi ya watu milioni 10.4 wakiwa wanaugua kifua kikuu. Kufuatia ugunduzi wa Robert Koch uliofanyika mwaka 1882, ugunduzi na utumiaji wa chanjo na dawa za kuponya kifua kikuu ulileta imani kuwa ugonjwa huu ungetokomezwa. Shirika la Umoja Wa Mataifa liliwahi kubashiri kuwa ugonjwa huu utakuwa umetokomezwa kufikia 2025.
Kifua Kikuu husababishwa na:
Ugonjwa wa kifua kikuu ama TB, husababishwa na bakteria aitwaye Mycobacterium tuberculosis. Bakteria huyu husambaa kwa njia ya hewa wakati mtu mwenye TB (ambaye mapafu yake yameshambuliwa) akikohoa,akipiga chafya,akitema mate,akicheka ,au akizungumza.
TB huambukizwa lakini siyo rahisi kuipata. Uwezekano wa kupata TB kutoka kwa mtu anayeishi au kufanya kazi naye ni mkubwa kuliko kutoka kwa mgeni. Watu wengi ambao tayari wamaeanza tiba sahihi angalau kwa wiki 2 hawaambukizi.
Toka antibiotics zilipoanza kutumika kutibu TB, baadhi ya aina ya bakteria hao wamegeuka sugu kwa dawa. Multidrug-resistant TB (MDR-TB) ni hali ambapo dawa haziwezi tena kuwaua bakteria wote, hivyo wale wanaosalia wanajijengea usugu wa dawa hiyo na dawa nyngine pia kwa wakati mmoja.
Multidrug-resistant TB (MDR-TB) inatibika kwa kutumia dawa za kipekee (very specific anti-TB drugs) ambazo ni chache na hazipatikani kirahisi. Katika mwaka 2012, karibu watu 450,000 walipata MDR-TB.
Watu wenye upungufu wa kinga za mwili huwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kupata active TB. HIV hudhoofisha kinga za mwili, na kuufanya mwili kupata shida ya kudhibiti bakteria wa TB. Watu wenye mchanganyiko wa HIV na TB wana uwezekano wa kupata active TB kwa kiwango cha ailimia 20-30 ukilinganisha na wale ambao hawana HIV.
Matumizi ya tumbaku yamedhihirika kuongeza uwezekano wa kupata active TB. Aslimia 20 ya TB duniani huhusishwa na matumizi ya tumbaku.
Dalili za manzo za Kifua Kikuu:
. Kukohoa, wakati mwingine kukiwa na makohozi au damu
. Kusikia baridi
. Uchovu
. Homa
. Kukonda kwa mwili
. Kukosa hamu ya kula
. Kutoa jasho usiku
Dalili za kifua kikuu:
Kifua kikuu huathiri hasa mapafu, lakini kinaweza kuathiri vile vile sehemu nyingine za mwili. Wakati TB imeathiri sehemu tofauti ya mwili, dalili zinaweza kubadilika. Bila kupata tiba, TB huweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili kupitia mfumo wa damu.
. Tb ikishambulia mifupa inaweza kuleta maumivu ya uti wa mgongo na kuharibu maungio ya mifupa
. TB ikishambulia ubongo husababisha meningitis
. TB ikishambulia maini na figo huweza kusababisha damu ndani ya mkojo
. TB ikishambulia moyo inaweza kuathiri uwezo wa moyo wa kusukuma damu na kusababisha cardiac tamponade ambayo inaweza kuua.
Tiba ya Kifua Kikuu
Wagonjwa wengi wa TB wanaweza kupona kama dawa stahiki itakuwepo na kutolewa inavyopaswa. Aina ya dawa na urefu wa muda wa matumizi vitategemea umri wa mgonjwa, hali yake ya afya kwa ujumla, usugu wa mwili wake kwa dawa, kama TB in latent au active, sehemu yake ya mwili iliyoathirika (i.e mapafu, ubongo, figo).
Watu wenye latent TB wanaweza kuhitaji aina moja tu ya dawa, wakati watu wenye active TB (na hasa MDR-TB) watahitaji mchanganyiko wa dawa.
Ni muhimu kwa mgonjwa kuhakikisha kuwa anamaliza dawa, hata kama dalili za TB zitakuwa zimeondoka. Bakteria waliosalia na kuvumilia tiba iliyotolewa wanaweza kugeuka sugu kwa tiba hiyo na kupelekea kupata MDR-TB hapo baadaye.

No comments