Mzozo mpya umeibuka kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya,
Mzozo mpya umeibuka
kati ya tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, na vinara wa mrengo wa
upinzani wa NASA kuhusu utangazaji wa matokeo rasmi ya kura za Urais.
IEBC
imeijibu mrengo wa upinzani wa Nasa kufuatia vitisho vyake vya kususia
uchaguzi iwapo tume hiyo itafaulu kwenye rufaa iliyowasilisha mahakamani
dhidi ya uamuzi wa mahakama ulioruhusu matokeo ya kura za Urais
kutangazwa katika kituo cha kupigia kura.
Hii ni baada ya
viongozi wa upinzani kuishauri IEBC dhidi ya kusaka njia za kubadili
mipango hiyo ili kutangaza matokeo ya kura za Urais katika kituo cha
kitaifa jinsi ilivyokuwa matokeo ya miaka iliyopita.
Tume hiyo
kupita mwenyekiti wake Wafula Chebukati, imeeleza kuwa haitobadili
msimamo wake wa kukata rufaa na kuwaambia viongozi wa upinzani kuheshimu
mahakama na kutumia njia za kisheria kutatua malalamiko yao.
Viongozi
wa mrengo wa upinzani wakiongozwa na Mgombea wa Urais, Raila Odinga,
walitishia kususia uchaguzi iwapo tume hiyo itakata rufaa na kuruhusu
matokeo ya Urais kutoka kila kituo kutangzwa kitaifa.
''Kuitishia
IEBC kuhusu uamuzi wake wa kukata rufaa, ni kutishia uhuru wake, na
wasioridishwa na hatua hiyo, wajiunge kwenye kesi wasake suluhisho za
kisheria,'' alisema Chebukati.
Taifa la Kenya linatarajiwa
kuandaa uchaguzi mkuu wa Urais baadaye mwaka huu huku ushindani mkali
ukitarajiwa kati ya Rais Uhuru Kenyatta anayewania kiti hicho kupitia
mrengo wake wa Jubilee na Raila Odinga, anayebeba bendera ya mrengo wa
Upinzani wa Nasa.
Takriban wagombea kumi na wanane wa Urais wamejitokeza.
Post a Comment