Mchezaji wa akiba Cesc Fabregas alifunga goli katika dakika ya 88
Mchezaji wa akiba Cesc Fabregas alifunga goli katika
dakika ya 88 wakati mabingwa wapya wa ligi kuu ya England, Chelsea,
walipowalaza Watford 4-3 usiku wa Jumatatu.
Mechi hiyo ya ligi iliyochezwa katika uga wa Stamford Bridge ilikuwa na mbwembwe chungu nzima.
Nahodha
wa the blues John Terry alicheza mechi yake ya 716 na akatia kimyani
bao la kwanza ila alifanya makosa na kumpelekea Etienne Capoue
kusawazisha. Cesar Azpilicueta na Mitchy Batshuayi walifunga baadaen na
kuwaweka Chelsea juu 3-1, lakini Stefano Okaka alifunga goli la
kusawazisha baada ya Daryl Janmaat kuwafungia Watford la pili.
Lakini
Cesc Fabregas alipachika wavuni goli la nne na kuwapa mabingwa hao
wapya ushindi na kuwaweka katika nafasi ya kuwa timu ya kwanza kushinda
mechi 30 katika ligi hiyo yenye mechi 38 kwa kila timu, lakini hilo
litafanyika iwapo watashinda mechi yao ya mwisho mnamo wikendi, kwani
kwa sasa wameshinda mechi 29.
"Kuna uwezekano wa kushinda mechi
30 na ni lazima tujaribu kulifikia lengo hilo sasa," alisema kocha wa
Chelsea Antonia Conte baada ya mechi hiyo.
Naye mkufunzi wa
Watford, Walter Mazzarri alisema, "kulikua na mazuri na ambayo si mazuri
katika mechi hiyo, lakini zaidi ya yote ninajivunia timu yangu."
Leo
hii kutakuwa na mechi zengine katika ligi hiyo ambapo Arsenal watakuwa
wanakwaana na Sunderland walioshushwa daraja tayari, mechi hiyo ikipigwa
uwanjani Emirates, halafu Manchester City wavae njuga kucheza na West
Bromwich Albion.
Post a Comment