Uhuru wa vyombo vya habari haujakmatukioomaa
Kila mwaka, tarehe 3 Machi, dunia inaadhimisha Siku ya
Uhuru wa Vyombo vya Habari. DW inaangalia hatua zilizopigwa na
changamoto zilizopo katika sekta ya habari barani Afrika kama vile
wanasiasa kuingilia sekta hiyo.
Huku dunia ikiadhimisha siku ya uhuru wa habari , waandishi habari
nchini Uganda wanazidi kukabiliwa na mazingira magumu ya kazi kutokana
na sheria kandamizi zinazobuniwa kila kukicha. Aidha makabiliano na
vyombo vya usalama hasa polisi na vitisho vya mara kwa mara kutoka kwa
wanasiasa na hata waajiri wao vimeshudiwa mara kwa mara. Haya ni licha
ya madai ya utawala nchini humo kwamba unalinda kwa dhati uhuru wa
habari.
Post a Comment