Trump amfuta kazi James Comey
Ikulu ya Marekani ya White House imetangaza jana kwamba rais Donald
Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la uchunguzi wa makosa ya
jinai FBI James Comey kuhusiana na jinsi
anavyoshughulikia uchunguzi
kuhusiana na barua pepe za Hillary Clinton. Barua kutoka Ikulu ya White
House imemfahamisha Comey kwamba kufukuzwa kwake kazi kunaanza mara
moja.
Comey amekuwa akiongoza uchunguzi kuhusu mawasiliano kati ya
wasaidizi wa kampeni ya Trump na maafisa wa Urusi kabla ya uchaguzi wa
rais mwaka 2016. Mkurugenzi huyo wa FBI
alikosolewa vikali pale
alipotangaza kwamba shirika lake linafungua upya uchunguzi kuhusiana na
jinsi Clinton alivyozihifadhi taarifa nyeti kiasi siku chache kabla ya
uchaguzi. Trump alisema katika barua yake kwamba Ikulu ya White House
tayari inatafuta mtu wa kuchukua nafasi yake.
chanzo dw
Post a Comment