MAJONZI tena Arusha.
MAJONZI
tena Arusha. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mti mkubwa kuserereka
umbali wa takribani mita 200 ukiwa umesimama kabla ya kuiangukia nyumba
walimokuwa wamelala ndugu watano wa familia moja na kuwaua wote.
Tukio
hilo limewakumbusha watu wa mkoa huo machungu ya kupoteza wanafunzi
33, walimu wawili na dereva wa gari la Shule ya Lucky Vincent ya mjini
hapa waliokufa kwa ajali ya gari wiki iliyopita baada ya basi lao kuacha
njia na kutumbukia korongoni wilayani Karatu.
Ikiwa
ni siku moja tu miili hiyo iagwe Uwanja wa Sheikh Amri Abedi mjini
hapa, ghafla watu watano wa familia ya Jonathan Kalamwia (55) mkazi wa
Kijiji cha Ng’ires, Kata ya Sokoni II wilayani Arumeru walifariki dunia
kwa kuangukiwa na mti mkubwa wakiwa wamelala usiku.
Ajali
hiyo iliyoacha simanzi na maswali mengi kwa wananchi wa Kijiji cha
Ng’ires na maeneo jirani, ilitokea saa 7.00 usiku wa kuamkia jana
wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Kwa
takriban wiki ya tatu sasa mvua nyingi imeendelea kunyesha mkoani hapa
yakiwamo maeneo ya milima na miinuko ya Mlima Meru ambako kipo Kijiji
cha Ng’ires.
Vyanzo
vya habari kutoka eneo la tukio vilisema iliwachukua zaidi ya saa 5.00
waokoaji kuitoa miili iliyokuwa imefunikwa na udongo.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema mti huo pamoja na miti mingine, ni wa asili na
wa siku nyingi na ulikuwa umeota kwenye Mlima Lakemana.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema wakati tukio hilo
linatokea, Mzee Kalambwia ambaye ni mlinzi katika Hospitali ya Dk.
Mohamed, alikuwa kazini.
“Juzi
Mei 9, mwaka huu usiku wakati mvua ikiendelea kunyesha katika Kijiji
cha Ng’eresi Kata ya Sokoni II, mti mkubwa uliserereka na kifusi cha
udongo na kufunika nyumba ya Kalambwia,” alisema Kamanda Mkumbo na
kuongeza:
“Ndani
ya nyumba walikuwa wamelala watoto wake watano ambao ni Gilead Jonathan
(31), Lazaro Namnyaki (26), Best Jonathan (20), Miriama Jonathani (16)
mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule Sekondari Enaboishu na
Gloria Jonathani (11) mwanafunzi darasa la tatu wa Shule ya Msingi
Ng’iresi.
“Haya
ni majonzi makubwa, huyu bwana kupotolewa na watoto wake wote. Mvua ni
baraka lakini kwa tukio hili limekuwa ni tatizo kubwa.
Nyumba
iliyokumbwa na ajali ipo kwenye bonde kwa hiyo mti ulitelemka ukiwa
umesimama na kuiangukia nyumba wakati familia ikiwa imelala.
“Niwaombe
wananchi kuchukua tahadhari mvua inayoendelea kunyesha ni wiki ya tatu
inanyesha mfululizo. Ni vema kila familia ichukue tahadhari ikiona
nyumba imelegalega ni muhimu waiimarishe, ikiwamo kupunguza miti
inayoonekana ni hatari”.
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Arusha, Wilson Mahera aliyekuwa kwenye eneo la tukio
hilo akishirikiana na wananchi, aliliambia MTANZANIA kuwa mti huo
ulisafisha kila kilichokuwa mbele yake, ulipokuwa ukiserereka.
“Kwa
kweli ni tukio la kusikitisha sana, ule mti umeng’oa kila kitu na
kutengeneza njia yenye upana kama wa mita 15 na ulisafisha kila
ulichokikuta njiani, tena ukiwa wima.
“Ulipofika
kwenye nyumba walimolala ndugu uliiangukia nyumba …miili ya wanawake
wawili imeharibika kutokana na kuangukiwa na mti huku wanaume wawili
wakiangukiwa na kuta na kukosa hewa akiwamo mmoja,” alisema Mahera.
Alisema
kutokana na tukio hilo kutokea usiku huku mvua ikiwa inaendelea
kunyesha, jeshi la polisi wakishirikiana na wananchi walifanikiwa
kutoa miili mitatu saa 11 afajiri huku miili mingine miwili ikitolea saa
2 asubuhi.
“Kule
milimani kuna miti mikubwa ya asili na kwa sasa katika eneo lile
imebakia mingine mitatu na wananchi wameomba kibali cha kuikata isije
kuleta maafa mengine kipindi hiki cha mvua nyingi.
“Lakini pia Serikali tumewaomba wananchi wote hasa waliojenga chini ya milima kuwa kuwa makini zaidi.
“Kutokana
na tatizo hili sisi halmashauri tutapeleka wataalamu wa washauri
wananchi namna ya kujenga nyumba zao hasa waliopo kwenye miinuko ya
milima,” alisema Mahera.
KAYA 80 ZAKOSA MAKAZI TANGA
Zaidi
ya kaya 80 nyumba zao zimezingirwa na maji huku nyingine zikihifadhiwa
katika shule kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa saa 24 jijini Tanga.
Madhara zaidi yamezikumba kata za Magaoni, Mzizima, Masiwani, Msambweni na Mzingani.
Wakazi wa maeneo hayo wamelazimika kuhama nyumba zao na kujihifadhi shuleni na wengine wakijihifadhi kwa ndugu zao.
MTANZANIA
lilishuhudia kata za Magaoni na Tangasisi ambazo awali zilikuwa
maarufu kwa uchimbaji wa mchanga, zikiwa zimeathiriwa kwa kiasi
kikubwana mafuriko wakati wa mvua.
Naibu
Meya wa Jiji la Tanga, Mohamed Haniu (CUF), alisema mvua hiyo
imesababisha athari zaidi kwenye madaraja ambayo mengi yamesombwa na
maji.
Mwenyekiti wa Magaoni B, Pendeza Hashim alisema athari imezidi kutokana na mifereji kuzidiwa na maji ya mvua.
Alisema
licha ya kuwapo miundombinu hiyo, l imeshindwa kusukuma maji
ikizingatiwa maji hayo yalikuwa mengi kushinda uwezo wa miundombinu
hiyo.
“Katika eneo langu tayari kaya 20 tumeweza kuzihifadhi katika shule ya msingi Magaoni baada ya nyumba zao kujaa maji.
“Baadhi ya wananchi waliiomba serikali kuharakisha msaada wa kibinadamu katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo,” alisema.
Mmoja wa waathirika wa mafuriko hayo, Zainabu Ramadhani alisema hawakuweza kuokoa chakula
wala nguo vyote vimekwenda na maji.
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Magaoni, Arafa Kibaya alisema wamelazimika
kusimamisha masomo jana kwa kuwa shule hiyo ilizingirwa na maji.
UMEME, MAJI HAKUNA
Wakati huohuo, wakazi wa Jiji la Tanga walikosa huduma ya umeme na maji kwa zaidi ya saa nane kwa sababu ya mvua hiyo.
Ofisa
Habari wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira, Dora Kilo,
alisema huduma ya maji imekosekana kutoka na kukosa umeme.
MAJI YAFUNIKA BARABARA
Kutokana
na mvua hiyo, jana barabara na madaraja katika maeneo ya Halmashauri ya
Chalinze mkoani Pwani yalifunikwa na maji ambayo yalikuwa yakikatisha
kwa kasi na kufanya usafiri kusimama kwa muda.
Mbali
na eneo pia mvua ilisimamisha shughuli kwa muda katika eneo la Mombo
wilayani Korogwe, ambako barabara ilifunikwa na maji huku baadhi ya
magari yakisombwa.
PEMBA HALI TETE
Kutokana
na mvua inayoendelea katika ukanda wa Pwani, hali katika Visiwa vya
Zanzibar imezidi kuwa tete baada ya mvua ya kuangusha miti, madaraja
na nyumba kisiwani Pemba jana.
Hali
hiyo inaelezwa kuwa ilisimamisha shughuli za uvuvi ambayo ndiyo kazi
kubwa ya wananchi, baada ya bahari kuchafuka hali ambayo ilisababisha
kitoweo hicho kuwa adimu.
Post a Comment