Marekani imeituhumu
serikali ya Syria kwa kujenga sehemu ya kuchoma maiti katika jela ya
kijeshi iliyopo karibu na Damascus ili kuficha mauaji ya halaiki ya
wanaoshikiliwa na serikali.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani
imeonyesha picha zilizopigwa kupitia njia ya Satelite ambazo imesema ni
sehemu ya kuchoma maiti katika gereza lililopo Sednaya ambapo Umoja wa
Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema maelfu ya
wafungwa wameteshwa na kunyongwa.
Mwanadiplomasia mwandamizi wa Marekani anayehusika
na masuala ya Mashariki ya kati, Stuart Jones, amesema kwa siku wafungwa
takriban hamsini wanauawa katika gereza la Sednaya.
Ameongeza kusema kuwa, mauaji hayo yanafanyika kutokana Syria kuungwa mkono na Urusi na Iran.
Post a Comment