Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva wa shule ya siku ya Lucky Vincent Jumamosi huko Karatu, Arusha.
RPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari
yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari.
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada
ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo
kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye
shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika
atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha.
Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu
30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.
Post a Comment