Tahadhari dhidi ya Ebola
Shambulio la mtandaoni duniani ambalo limesababisha kutekwa kwa mafaili
katika kompyuta linaonekana kupungua kuanzia jana Jumatatu wakati
maafisa wanafanyakazi kuwakamata watu
wanaohusika. Miongoni mwa
waliyogundua ni uwezekano wa uhusiano kati ya kirusi kinachofahamika
kama "ransomware", kinachotambulika kama WannaCry na wadukuzi ambao
wanahusiana na Korea kaskazini. Ugunduzi huo bado ni wa muda , kampuni
moja ikiueleza kuwa ni njama lakini bado ni dhaifu.
Kampuni ya usalama
wa mtandaoni Kaspersky Lab imesema kwamba sehemu ya programu ya WannaCry
inatumia mfumo wa kanuni kama malware ambayo ilisambazwa hapo kabla na
kundi la Lazarus, kundi la wadukuzi ambao walihusika na kudukua mafaili
ya kampuni ya Sony ambalo Korea kaskazini ililaumiwa.
Wakati huo huo
rais wa Urusi Vladimir Putin amesema kwamba Urusi haihusiki kwa lolote
na shambulio hilo la mtandaoni.
Post a Comment