Donald Trump amefichua taarifa za siri
Gazeti la Washington Post limeripoti kwamba rais Donald Trump amefichua
taarifa za siri kuhusiana na wanamgambo wa Dola la Kiislamu kwa maafisa
wa Urusi wakati wa mkutano wao wiki
iliyopita, na kusababisha shutuma
kali kutoka kwa Wademocrats na Warepublican. Mshauri wa usalama wa taifa
McMaster alizungumza na waandishi habari kukana taarifa hizo.
"Hakuna
kitu ambacho rais anakichukulia kwa dhati kabisa kama usalama wa watu wa
Marekani. Taarifa hiyo imekuja usiku, kama ilivyoripotiwa, ni uongo.
Rais na waziri wa mambo ya kigeni
wameangalia vitisho kadhaa kwa nchi
zetu mbili ikiwa ni pamoja na kitisho kwa usafiri wa anga. Hakuna wakati
vyanzo vya
upelelezi ama mbinu vilijadiliwa."Gazeti hilo la Washington
Post limesema mshirika wa upelelezi hakutoa ruhusa kwa Marekani kutoa
taarifa hizo kwa maafisa wa Urusi. Shirika la ujasusi la Marekani CIA na
ofisi ya mkurugenzi wa idara ya upelelezi ya taifa walikataa kusema
lolote jana.
chanzo dw
Post a Comment