Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru
Mmoja wa wasichana
wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua
kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais
wa Nigeria.
Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.
Garba
Shehu aliambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa
huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.
- Buhari na Wasichana wa Chibok
- Wasichana wa Chibok waungana na familia
- Video 'yaonyesha wasichana wa Chibok waliotoweka'
Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.
Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na uhuru wa wasichana hao duru ziliambia BBC.
Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.
Post a Comment