Header Ads

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano

MULIRO JUMANNE MULIRO 


Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuwabaini na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote wanaojihusisha na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na wale wanaouza pombe aina ya Viroba.

Akizungumza na RADIO FARAJA FM STEREO kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga MULIRO JUMANNE MULIRO amesema wakati jeshi hilo likiendelea na oparesheni maalum ya kukabiliana na biashara hizo wananchi wanapaswa kuonyesha ushirikiano kwa kutoa taarifa za kweli ambazo zitasaidia kuwakamata na kuwafikisha watuhumiwa katika vyombo vya sheria.
.
Akizungumzia kuhusu dawa za kulevya amesema, kwa sasa jeshi la polisi limejikita zaidi kuwatafuta wasambazaji wa dawa hizo ambapo mpaka sasa linawashikilia watu zaidi ya kumi, huku wachache kati yao wakiwa wamefikishwa mahakamani na wengine wanaendelea kuhojiwa.

Kamanda MULIRO amepongeza hatua ya  wananchi wengi kuungana na jeshi la polisi kwa kuonyesha kukerwa na dawa za kulevya baada ya kushuhudia zikiendelea kuleta madhara makubwa kwa watoto na ndugu zao.

No comments