Staa wa Man United amempoteza binamu yake kwa kupigwa risasi
March 6 2017 inaweza kuwa siku mbaya kwa staa wa Man United na shabiki wa Man United kutokana na staa wa timu hiyo Marcos Rojo kumpoteza binamu yake aliyepigwa risasi huko kwao Argentina kwa tuhuma za unyang’anyi.
Beki wa Man United amepokea taarifa za kuuwawa kwa binamu yake Geronimo Rojo mwenye umri wa miaka 17, kwa kudaiwa kujaribu kufanya uporaji akiwa kwao Argentina Jumatatu ya March 6, Geronimo alipigwa risasi alipojaribu kumpora askari msataafu.
Geronimo amefariki akiwa hospitali lakini wakati wa tukio alikuwa katika pikipiki na mwenzake Ivan Rodrigo Barbosa mwenye umri wa miaka 26 ambaye alipigwa risasi na kufariki katika eneo la tukio wakati wakijaribu kufanya uporaji.
Post a Comment