Wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutunza miundo mbinu
Wananchi katika Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kutunza miundo mbinu ya serikali hali itakayosaidia kuonyesha Mandhari nzuri ya Mpango Mji.
Hayo yameelezwa na afisa mipango miji wa Manispaa ya Shinyanga bwana Emanuel Mitinje kwenye Mkutano wa hadhara uliohusisha Maafisa wa idara ya ardhi kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu kuzitambua sheria na taratibu za hati miliki ya ardhi.
Bwana MITINJE amefafanua kuwa wananchi wanao wajibu mkubwa kuhakikisha wanaheshimu miundo mbinu ya serikali ikiwemo reli ili kurahisisha utaratibu wa uainishaji na mandhari nzuri ya Mji kwa mujibu wa Sheria za ardhi.
Amesema wananchi wanapaswa kutambua kwamba utaratibu wa ubadilishaji makazi unatakiwa kuzingatia sheria ya mipango miji ili kudhibiti migogoro ya ardhi.
Akifafanua kuhusu sheria za ardhi afisa huyo amesema kuwa wananchi wanapaswa kurudisha ofa ili utaratibu wa kupatiwa hati miliki uweze kufanyika kwa kuzingatia mwongozo uliotolewa na wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi,ikiwa ni Pamoja na namna ya kulipia gharama.
Mwenyekiti wa mtaa wa Dome Solomon Nalinga amewaomba wakazi wa mtaa huo kujua,kuheshimu na kufuata sheria za ardhi zinazotolewa na maafisa ardhi.
IDARA YA ARDHI KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA IMEENDELEA NA ZOEZI LA KUELIMISHA JAMII KUHUSU SHERIA NA TARATIBU ZA MIPANGO MIJI IKIWA NI UTEKELEZAJI WA AGIZO LILILOTOLEWA NA WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI,WILLIAM LUKUVI.
Post a Comment