Rapper Harmorapa amekutana uso kwa uso na msanii mkongwe wa muziki Haule aka Professor Jay
Rapper Harmorapa amekutana uso kwa uso na msanii mkongwe wa muziki wa hip hip ambaye pia ni mbunge wa Mikumi Joseph Haule aka Professor Jay na kumuonyesha mkongwe huyo kile anachokifanya kwenye muziki wa hip hop.
Wawili hao walikutana wiki iliyopita katika studio ya Parazobeats ya producer Mr Ttouch iliyopo Sinza Parestina jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa video hiyo, Mr T touch alimuamuru Harmorapa kuchana kidogo ili Professor J aone kipaji cha kijana huyo.
Post a Comment