Ukosefu wa dhana bora za kilimo na ukosefu wa elimu juu ya kuongeza thamani ya mazao
Ukosefu wa dhana bora za kilimo na ukosefu wa elimu juu ya kuongeza thamani ya mazao umetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa wanannchi wa pembezoni kushindwa kulima kilimo cha kisasa hali inayochangia kuwepo kwa uhaba wa chakula kila mara
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na wakulima kutoka kata ya Mwadui Lohumbo kwenye kikao kilichofanyika wilayani kishapu chini ya mtandao wa jinsia tgnp wakati kikundi cha taarifa na maarifa kikiwasilisha changamoto mbali mbali zinazowakabili katika kata yao
Taarifa ya kituo hicho iliyowasilishwa na bi LUCIA DAUD imesema kuwa changamoto ya dhana bora za kilimo ,soko pamoja na wanaume kutojihusisha na kilimo huchangia kukosa mazao ya kutosha kwa ajili ya chakula na biashara na kuiomba serikali kuwapatia elimu juu ya kilimo cha kisasa na kuwatafutia masoko
Godwin everygis ni kaimu afisa kilimo wa wilya ya shinyanga amekiri kuwepo kwa tatizo la ukosefu wa elimu kwa wakulima kutokana na idadi ya wataalamu kuwa ndogo katika halmashauri hiyo huku akibainisha hatua wanazochukua kuwasaidia wakulima hao
kikao hicho kilichoandaliwa na tgnp mtandao kimewashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo pamoja na wakuu wa idara za halmashauri hiyo
Post a Comment