Klabu ya Yanga imepigwa faini ya Tsh 500,000
Klabu ya Yanga imepigwa faini ya Tsh 500,000 (Laki Tano) kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mechi yao dhidi ya Simba iliyopigwa uwanja wa Taifa Feb,25,2017.
Timu hiyo wamepata faini hiyo baada ya kamati ya Bodi ya Uendeshaji na usimamizi wa ligi Tanzania (Kamati ya Saa 72) kukaa kikao Machi,4,2017 ili kupitia matukio mbalimbali ya ligi kuu Tanzania Bara msimu huu.
Imeelezwa kuwa kitendo hicho walichofanya Yanga ni kinyume cha kanuni ya 14(14) ya ligi kuu inayosema kuwa timu zitaingia uwanjani kwa kutumia milango rasmi.
Post a Comment