Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania , Mbarouk, Mwarija, na Mkuye wameahirisha rufaa hadi Februari, 27
Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania , Mbarouk, Mwarija, na Mkuye wameahirisha rufaa hadi Februari, 27 mwaka huu iliyokatwa na wapiga kura wanne wa Jimbo la Bunda Mjini kupinga matokeo ya uchaguzi dhidi ya Mbunge wa jimbo hilo Ester Bulaya (Chadema)
Rufaa hiyo ilikatwa na Wapiga kura Magambo Masato, Matwiga Janes, Ezekiel na Ascetic Malagila, wanaoiwakilishwa na wakili Costantine Mutalemwa imeanza kusikilizwa jana jijini hapa.
Awali kwa upande wake mjibu rufaa ambaye Esta Bulaya akiwakilishwa na wakili Tundu Lissu alisema hayuko tayari ,kuruhusu mahakama kuendelea na rufaa hiyo kutokana hoja ya rufaa hivyo kuhitaji umakini na ueledi wa hali ya juu hivyo kuomba kuongezewa wa muda wa kuisoma na kueilewa.
“Mheshimiwa Jaji kutokana na kifungu Namba 106 kanuni ndogo ya (8) kuruhusu siku 30 toka rufaa ilivyokatwa, nami naomba iwe hivyo kwani toka Februari 11 mwaka huu siku 30 bado,” alieleza Lissu
Lissu pia alisema rufaa hiyo ameipata kimakosa kwani alitumiwa na kijana mmoja wakili wa hapa Mwanza Paul Kipeja kwa njia ya barua pepe angali waleta rufaa wanajua sina Ofisi Mwanza hivyo kusamehe hayo makosa bila malipo.
Lissu aliongeza kuwa kutokana na sababu za hoja hizo ameiomba Mahakama kama itahairisha kesi hiyo ili kumpatia nafasi ya kujiandaa vya kutosha ili kuweza kujibu hoja za wakata rufaa.
Jaji wa Rufani Mbarouk alihoji endapo Lissu atakubaliwa hoja yake haoni kuwa rufaa hii itachukua muda mrefu kumalizika kutokona na kifungu namba 109 (19) kuruhusu kesi za uchaguzi mahakama ya rufani kuharakishwa.
Akijibu hoja hiyo Lissu alisema kuwa Sheria ya kesi za uchaguzi mahakama ya Rufani inapswa kusikilizwa kwa mwaka mzima hivyo hoja ya kifungu namba 109 (19) hakina mashiko badala yake itumike busara kutumia kifungu cha awali.
Aidha Lissu aliiomba Mahakama hiyo kama itahiari rufaa hiyo iamishiwe Dar es Salaam kwa kuwa amekubaliana na mawakili wa wakata rufaa juu ya jambo hilo.
Akijibu hoja za Lissu wakili wa upande wa mkata rufaa Costantine Mtalemwa alisema kuwa anapingamizi juu ya hoja za mjibu rufaa hiyo kwani ni haki yake kisheria kupewa siku 30 na bado yuko ndani ya muda.
Wakihairisha rufaa hiyo jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani Tanzania ambao ni Mbarouk, Mwarija, na Mkuye wakiongozwa na Mbarouk alisema kuwa Mahakama itamua Rufani hiyo itaendelea kusikilizwa kati ya Mwanza ama Dar es Salaam kama hoja za mawakili zilivyosema.
na mwandishi wetu wakali zote blog Harity Timberland kutoka Mwanza
Post a Comment