Wanawake Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa Mabalozi
Kutokana na nafasi yao katika Jamii Wanawake Mkoani Shinyanga wametakiwa kuwa Mabalozi na mfano Bora wa kuzingatia sheria,kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kudhibiti ajali.
Akizungumza katika hafra ya siku ya familia ya Polisi katika ukumbi Mpya wa NSSF Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ZAINABU TELACK amesema kutokana na umakini wa wanawake na nafasi waliyo nayo katika Jamii wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhamasisha wengine kuhusu madhara ya kukiukwa kwa sheria za usalama barabarani.
Aidha ameliagiza Jeshi la Polisi kuchukua hatua za kisheria kuwashughulikia wale wote watakaokaidi kuheshimu na kufuata kanuni na taratibu za usalama barabarani.
Mkuu wa Mkoa amesema vyombo vya dola havitosita kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya mwananchi atakayebainika kukiuka sheria na kanuni za usalama barabarani.
Post a Comment