Header Ads

Jeshi la Polisi Mkoani shinyanga,kufanikiwa katika utendaji wake wakazi

MURILO JUMANNE MURILO

Imebainishwa kuwa kuzingatiwa kwa misingi ya sheria,haki na usawa katika kazi ni Mambo ya Msingi yaliyosababisha Jeshi la Polisi Mkoani shinyanga,kufanikiwa katika utendaji wake.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi MURILO JUMANNE MURILO ameyasema hayo kwenye sherehe ya kuwaaga askari waliostaafu kazi,iliyokwenda sambamba na siku ya familia ya Polisi,kuaga mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017

Kamanda MURILO amesema hatua za mafanikio za Jeshi hilo zimetokana na uadilifu wa askari wake wakiwemo waliostaafu kwa kushirikiana na wananchi
Amesema Jeshi hilo linatambua na kuthamini mchango mkubwa wa askari wastaafu  katika  usalama na ujenzi wa Taifa.

                
Akizungumza katika hafra hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ZAINABU TELACK ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Shinyanga ambao wameendelea kuunga mkono Jitihada za Jeshi la Polisi na kamati ya ulinzi na usalama.
 aidha, amesema serikali ipo bega kwa bega na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika Jamii,ambapo pia  amewapongeza wastaafu wa Jeshi hilo na kusema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wao katika ustawi wa Taifa.
                      
Amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kutoa taarifa sahihi zitakazosaidia kuwabaini na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahalifu.
                      

No comments