Header Ads

ally kiba hawanjia ya mzungu kupenya see vidio



Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Israel Gilard Millo, amesema msanii wa bongo fleva Alikiba ndiye aliyemu-'insipire' kuimba Kiswahili, kitu ambacho kimempa mafanikio makubwa.



Akizungumza kwenye kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Television, Gilard ambaye hivi sasa ametua bongo, amesema wimbo wa 'Cinderela' wa Alikiba ndio ulimfanya azidi kupenda kuimba kwa lugha ya Kiswahili, baada ya kuona mashabiki wakimshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo huo jukwaani. 
"Cinderela ndio wimbo ulionifanya mimi nianze kuimba Kiswahili, nilikuwa nauimba na band live, na ndio wimbo wa kwanza wa Kiswahili nilioanza kuimba, sasa nikiimba watu wakawa wanashangilia huyu ni mzungu lakini anaimba Kiswahili, nikapenda nikaanza kuimba na zingine kwa Kiswahili, na mpaka leo naimba nyimbo zangu kwa Kiswahili", amesema Gilard.
Gilard ana kazi mbali mbali ambazo zimemfanya achukue tuzo za kimataifa, ambazo zimeimbwa kwa lugha ya Kiswahili, ikiwemo Unajua, Nairobi Yangu, Mapenzi, Sema milele na nyinginezo.
Tazama hapa moja ya kazi zake 

No comments