Klabu ya soka ya Simba imejipanga kutetea ubingwa wake
Klabu ya soka ya Simba imejipanga kutetea ubingwa wake wa kombe la shirikisho, ambapo leo itaanza rasmi mbio hizo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Green Warriors ya Dar es salaam.
Kuelekea mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 1:00 usiku, klabu ya Simba imewataka mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kwenye uwanja huo ili kuipa nguvu klabu yao katika safari yake ya kutetea ubingwa.
Mchezo huo wa leo ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo msimu huu, ambayo ilianza miezi miwili iliyopita katika hatua za awali lakini Simba ndio mabingwa watetezi na walitwaa ubingwa huo kwa kuifunga Mbao FC 2-1 katika fainali iliyopigwa Mei mwaka huu mjini Dodoma.
Leo pia kutakuwa na michezo mingine ambapo Polisi ya Dar es Salaam itamenyana na Mgambo JKT ya Tanga, Kariakoo ya Lindi dhidi ya Transit Camp ya Dar es Salaam, Biashara ya Mara na Mawenzi Market ya Morogoro, Ruvu Shooting ya Pwani na Madini FC ya Arusha, Mufindi United na Pamba ya Mwanza huku Singida United itacheza na Boda Boda FC.
Post a Comment