Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johnson amesema kuwa anatarajia
kuelezea kuguswa kwao kutokana na kufungwa kwa mwanamke raia wa Uingereza mzaliwa wa Iran Bi Zaghari-Ratcliffe akituhumiwa kuwa ni mpelezi tuhuma ambazo alizikanusha.
Waziri Johnson anatarajiwa kushinikiza kuachiwa huru kwa mwanamke huyo ambaye anatumikia kifungo cha miaka mitano jela.
Hii ni ziara ya kwanza ya Boris Johnson nchini Iran,ambayo inakuja wakati ambapo kuonaongezeko la hali ya wasiwasi mashariki ya kati.
Mambo mengine anayotarajia kuyazungumzia Johnson akiwa nchini Iran,ni pamoja na ushiriki wa Iran katika mzozo wa Syria and Yemen.
Mwandishi wa masuala ya Kidplomasia James Robbins anasema ziara ya Johnson Tehran,ni tatu tangu ile iliyofanywa na waziri wa mambo ya nje wa Uingereza mwaka 2003.
Post a Comment