Header Ads

Rais wa zamani wa Chile Sebastian Pinera, ameshinda kwa mara nyingine


Rais wa zamani wa Chile Sebastian Pinera, ameshinda kwa mara nyingine katika uchaguzi wa urais na kulirejesha taifa hilo kwa wafuasi wa mrengo wa kulia lakini pia ikiashiria kuongezeka kwa idadi ya viongozi wa kihafidhina wanaoshinda katika bara la Amerika Kusini.
 Huku karibu kura zote zikiwa zimehesabiwa, bilionea huyo anaonekana kushinda kwa asilimia 54.6 katika uchaguzi uliofanyika jana Jumapili dhidi ya mpinzani wake mwandishi wa habari wa zamani na mfuasi wa siasa ya mrengo wa wastani wa kushoto, Alejandro Guillier aliyepata asilimia 45.4. 
Wachambuzi walibashiri kuwepo kwa kinyang'anyiro kikali wakidhani Guillier alikuwa amepiga hatua kubwa ingawa hakukufanyika uchunguzi wowote wa maoni tangu duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika mwezi Novemba. Pinera aliyeangazia zaidi kuimarisha uchumi wa taifa hilo linalozalisha kwa kiasi kikubwa madini ya shaba duniani amewashukuru wapinzani wake na kutoa mwito wa umoja.

No comments