Waziri mkuu wa zamani wa Lebanon , Saad Hariri, yuko nchini Ufaransa ambako anatarajiwa kuzungumza na rais Emmanuel Macron kuhusu swala tata la kujiuzulu kwake.
Hariri alikuwa Saudia wiki mbili zilizopita ambako ndiko alikotoa tamko la kujiuzulu wadhfa wa uwaziri mkuu akisema alikuwa anatishiwa maisha huko nchini mwake Lebanon na kundi la watu wenye ushirika mkubwa na Iran.
Awali maafisa wa Lebanon walikuwa wamedai kwamba Hariri anazuiliwa huko Saudia jambo ambalo alilikana vikali , akisema anachofanya ni maamuzi binafsi.
Swala lengine kuu lilikuwa ni vipi na lini atarudi Beirut.
Imeripotiwa amemweleza rais Michel Macroun kwamba atarudi nchini Lebabon Jumatano wiki hiii.
Kivyovyote vile safari hii ya Ufaransa inafungua ukurasa mpya katika hali ya kupimana nguvu kwenye mvutano baina ya Iran na Saudia ambao umekuwa ukijitokeza kwa namna tofauti katika maeneo tofauti ambako mataifa hayo mawili yanaendeleza ushawishi na maslahi yao kama vile Lebanon, Qatar, Syria na Yemen.
Post a Comment