Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo hii litapigia kura muswada wa azimio unaopinga hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel, duru za kidiplomasia zimearifu.
Misri iliomba kura hiyo jana Jumapili siku moja baada ya ya kuwasilisha azimio ambalo linaweza kupigiwa kura ya turufu na Marekani.
Akikaidi sheria na makubaliano ya kimataifa Trump alitangaza mwanzoni mwa mwezi huu kwamba anaitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel na kwamba Marekani itahamishia ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda mji huo, hatua iliyoamsha maandamano na kulaaniwa vikali.
Makamu wa Rais Mike Pence atazuru Jerusalem Jumatano hii kwa kile Ikulu ya Marekani inachosema ni kusaka njia ya kuanzisha tena mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati ingawa tayari Palestina imetangaza kutokushirikiana tena na Marekani.
Post a Comment