Header Ads

KINANA KUENDELEA KUONGOZA CCM

Image result for picha ya kinana

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania Abdurahman Kinana ataendelea kuwa katibu mkuu wa chama hicho.
Taarifa kwamba ataendelea kuhudumu zimepokelewa kwa shangwe na vigelegele na wajumbe wanaohudhuria mkutano mkuu wa tisa wa chama hicho mjini Dodoma.
Rais Magufuli ambae ndiye mwenyekiti wa sasa, alitangaza uamuzi huo wa Bw Kinana kwa wajumbe hao takriban 1,900.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Dkt Magufuli alimshukuru katiba mkuu wake na kusema ana imani naye katika utendaji wake wa kazi.

Punde tu baada ya kauli hiyo kutolewa, wajumbe takriban wote walisimama huku wakipiga makofi na wengine wakisema, "Jembe, Jembe."
Bw Kinana ambaye amekuwa akishikilia wadhifa huko tangu serikali ya awamu ya nne, na wachambuzi wamekuwa wakimuona kama kiungo muhimu sana katika kuleta mabadiliko ndani ya Chama.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba Kinana angeachia nafasi hiyo kwa lengo la kutaka kustaafu.
Kinana, mbali ya kuwa mwanajeshi mstaafu, ana uzoefu mkubwa katika masuala ya utawala na siasa.

No comments