Header Ads

Wahanga na familia za watu waliouawa kwenye shambulizi la lori

Image result for picha ya wahanga


Wahanga na familia za watu waliouawa kwenye shambulizi la lori katika soko la Krismas mjini Berlin mwaka jana watakutana kwa mara ya kwanza na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani wakati kukiwa na ghadhabu dhidi ya serikali yake kwa kushindwa kuzuia shambulizi hilo na namna ilivyolishughulikia.

Mkutano wa leo hii ulitangazwa muda mfupi baada ya majeruhi na familia ya waliouawa kumtumia Kansela Merkel barua ya wazi, wakimueleza kiongozi huyo wa muda mrefu kwamba lingelikuwa jambo la heshima kukutana nao muda mfupi baada ya tukio hilo.

 Kundi hilo pia limeangazia masuala rasmi pamoja na taarifa za vyombo vya habari zikionesha namna ambavyo idara nyingi za serikali zilivyovuruga ufuatiliaji wa mshambuliaji Anis Amri raia wa Tunisia aliyekuwa akiomba hifadhi na mhalifu wa makosa madogo ambaye polisi ya Ujerumani ilimuhisi kuwa na mahusiano na makundi ya itikadi ya Kiislamu. Familia hizo zitazindua kumbukumbu kesho Jumanne kuwakumbuka watu 12 waliouawa kwenye shambulizi hilo.

No comments