Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kukamilisha usajili
Klabu ya soka ya Singida United imethibitisha kukamilisha usajili wa beki wa kati kutoka timu ya taifa ya Ghana, Malik Antri.
Malik Antri akiwa katika majukumu ya timu ya taifa ya Ghana
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa timu hiyo kupitia mtandao wa Twitter imesema, mchezaji huyo amesajiliwa kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Elisha Muroiwa wa Zimbabwe ambaye ametimkia kwao kutokana na matatizo ya kifamilia yanayomkabili.
Malik Antri (wapili kutoka kulia) akiwa na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ghana
“Tunapenda kuwafahamisha kuwa tumekamilisha usajili wa beki wa kati wa timu ya Taifa ya Ghana (CHAN) Ndg. Malik Antri ambaye hii leo amewasili Singida. Malik Antri amchukuq nafasi ya Elisha Muroiwa aliyerejea kwao Zimbabwe kufuatia matatizo ya kifamilia yanayomsumbua,” imesema taarifa hiyo.
Kwa sasa Singida United inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 20, imecheza michezo 11 huku ikiwa imefungwa mechi moja, sare michezo mitano na kushinda michezo mitano.
Post a Comment