Header Ads

MTU WAWATU

Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama (Kushoto) na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje, Hillary Clinton.
Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama na aliyekuwa mgombea urais kwa tikiti ya chama cha Demokratik, Hillary Clinton, bado ndio watu wawili wanaopendwa sana na Wamarekani, kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanywa na kampuni ya utafiti ya Gallup.
Uchunguzi huo wa maoni unaonyesha kwamba wawili hao wameendelea kushikilia taji hilo kwa miaka kumi mfululizo, licha ya kwamba umaarufu wao umepungua kwa kiasi, ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Asili mia 17 ya wale waliohojiwa walisema Obama ndiye mwanaume anayependwa sana akilinganishwa na rais Donald Trump aliyechukua nafasi ya pili akiwa na asilimia 14 ya umaarufu.
Bi Clinton, ambaye kwa wakati mmoja alikuwa waziri wa mambo ya nje, alimshinda mkewe Obama, Michelle Obama. Clinton alikuwa na asili mia 9 huku Bi Obama akiwa na asili mia 7.
Huu ni mwaka wa 16 mfululizo kwa kura hiyo ya maoni kumwonyesha Hillary Clinton kama mwanamke anayependwa mno.

No comments