mataifa 128 yamepiga kura kuunga mkono mswada
mataifa 128 yamepiga kura kuunga mkono mswada
Katika kikao cha dharura cha baraza kuu la Umoja wa Mataifa jana, mataifa 128 yamepiga kura kuunga mkono mswada wa azimio unabatilisha uamuzi wa rais wa Marekani Donald Trump kuutangaza mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Baada ya kura hiyo, balozi wa Marekani katika Umoja huo Nikki Haley ameyashukuru mataifa 65 ambayo yamepinga azimio hilo, yamejizuwia kupiga kura ama hayakuwapo wakati wa kupiga kura.
Marekani na nchi jirani ya canada na Mexico zilijizuwia kupiga kura , pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya mashariki ikiwa ni pamoja na Poland, Jamhuri ya Cheki na Romania.
Kabla ya kura hiyo, Marekani ilitishia kupunguza misaada ya kifedha kwa nchi zitakazopiga kura kuunga mkono azimio hilo kwamba Jerusalem ni suala litakaloamuliwa kupitia majadiliano ya amani na Wapalestina na Israel.
Haley amesema kura hiyo haitabadilisha kitu katika mipango ya Marekani kuhamishia ubalozi wake mjini Jerusalem kutoka Tel aviv, lakini italeta tofauti kwa Wamarekani watakavyouangalia Umoja wa Mataifa na vipi wataziangalia nchi , kama alivyosema "zisizoiheshimu Marekani na Umoja wa Mataifa.
Post a Comment