Header Ads

serikali ya congo pamoja na Umoja wa Mataifa wajadiliana

Image result for PICHA YA WANAJESHI WA UN
usalama na uchaguzi mpya nchini humo.Awali, Lacroix alitembelea mji wa Goma siku ya Ijumaa, na kuwaangalia walinda amani 30 waliojeruhiwa katika shambulio lililotokea katika mji wa Kivu Kaskazini, mnamo Desemba 7 mwaka huu.
Chanzo kimoja cha habari kilicho karibu na majeshi ya kulinda amani nchini Congo, MONUSCO, kimeliambia shirika la habari la AFP kuwa Kabila na Lacroix  walijadili kuhusu shambulio hilo, ambalo ni baya kabisa katika historia ya karibuni ya majeshi hayo.
Lacroix alisema machafuko katika upande wa mashariki wa Congo ni mrundikano wa matatizo ambayo yanahitaji kufanyiwa kazi kwa pamoja. "Ushirikiano na nchi jirani ni muhimu sana," amenukuliwa Lacroix akizungumza kwenye Redio ya Umoja wa Mataifa.
Eneo kubwa la mashariki mwa Congo, limekabiliwa na machafuko kwa muda mrefu, lakini mapigano baina ya majeshi ya serikali na makundi ya wanamgambo, pamoja na mapambano ya kikabila yameongezeka zaidi mwaka huu.
Jimbo la Kivu Kaskazini, ambalo lipo mpakani mwa Uganda na Rwanda, limekabiliwa na mauaji  kwa kiasi kikubwa na utekaji nyara baina ya makundi ya waasi na ya kikabila.
serikali mjini  Kinshasa pamoja na Umoja wa Mataifa kwa kuua watu zaidi ya 700 katika mji wa Beni, ambako shambulizi jingine limefanyika wiki iliyopita.
Nchi hiyo pia inakabiliwa na machafuko kutokana na Rais Kabila kugoma kutoka madarakani baada ya muhula wake wa mwisho kufika mnamo Desemba mwaka jana, huku akiusogeza mbele uchaguzi hadi Desemba 2018.
Lacroix amesema, mchakato huo ni wajibu wa viongozi wa Congo. Alisema UN imeonyesha dhamira ya kushiriki katika mchakato huo.Siku moja baada ya shambulio hilo, Lacroix alinukuliwa na shirika la habari la AP akisisitiza kuwa lengo la walinda amani hao ni kulinda raia.
Awali akiwa katika hospitali ya Goma, Lacroix aliwaambia walinda amani waliojeruhiwa katika shambulio la Desemba 7 kuwa amekwenda Tanzania pia  na kwamba kwamba nchi hiyo ipo pamoja nao.
Lacroix alikuwa jijini Dar es Salaam Alhamis ya wiki iliyopita na kutoa heshima zake za mwisho kwa walinda amani 14 wa Tanzania waliouawa katika tukio hilo. Walinda amani watano wa Congo waliuawa pia katika shambulio hilo, lililowajeruhi wengine 53.

No comments