Header Ads

Al-Shabab washambulia mtambo wa mawasiliano Kenya

Shabab


Image copyright AFP
Image caption Wanamgambo wa al-Shabab wamekuwa wakishambulia Kenya mara kwa mara
Washukiwa wa kundi la Al-Shabaab mapema leo Alhamisi wameshambulia na kulipua mtambo wa mawasiliano ulioko katika mji wa Fino, Lafey katika kaunti ndogo ya Mandera nchini Kenya.
Afisa mkuu wa Polisi huko Lafey, Bosita Omukolongolo, amesema kuwa kisa hicho kilitokea saa nane usiku.
Afisa huyo wa Polisi anasema kuwa walikabiliana vikali na wanamgambo hao, lakini hakuna maafa yaliyoripotiwa upande wa polisi waliokuwa wakiulinda mlingoti huo wenye vifaa vya kupeperusha mawasiliano.
Kundi la Al- Shaabab, ambalo lina makao yake nchini Somalia, limehusika na mashambulizi ya mara kwa mara pamoja na mauaji nchini Kenya na mataifa kadhaa ya Afrika Mashariki na upembe wa Afrika.

No comments