Header Ads

SportPesa ya Kenya kudhamini klabu ya EPL


Hull CityImage copyrightREUTERS
Image captionHull City watafungua msimu dhidi ya mabingwa Leicester
Kampuni ya mashindano ya bahati nasibu inayodhamini Ligi Kuu ya Kenya imetia saini mkataba wa kuwa mdhamini wa klabu ya Hull City ya Uingereza.
Kampuni hiyo ya SportPesa, ambayo huandaa mashindano ya kubashiri matokeo ya mechi nchini Kenya, imetia saini mkataba wa kudhamini Hull City kwa misimu mitatu.
Klabu ya Hull City ilifanikiwa kurejea kwenye Ligi ya Premia msimu utakaoanza mwezi ujao.
Hull City watafungua msimu kwa mechi ya nyumbani dhidi ya mabingwa Leicester City.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa klabu hiyo, udhamini wa SportPesa ndio wa juu zaidi kuwahi kupokelewa na klabu hiyo katika historia yake ya miaka 112.
Hull City imekuwa ikidhaminiwa na kituo cha burudani cha Flamingo Land.

No comments