Header Ads

Daktari Feki Adaiwa Kuua Mgonjwa Baada ya Kumfanyia Upasuaji wa Tezi Dume Huko Singida

Mkazi mmoja mkoani Singida anayedaiwa kuwa daktari feki anatuhumiwa kusababisha kifo cha mgonjwa, Israel Shabani (68) baada ya kumfanyia upasuaji wa tezi dume. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita saa mbili usiku nyumbani kwa mtuhumiwa baada ya kumfanyia Shabani upasuaji. 


Alisema mtuhumiwa huyo anadaiwa alikuwa akifanya kazi katika vituo vya afya serikalini, lakini baada ya kuacha alijiita daktari na kuamua kutoa tiba ikiwamo ya upasuaji nyumbani kwake kinyume na sheria. 


Baada ya kumfanyia upasuaji huo wa kienyeji, mgonjwa huyo alitokwa damu nyingi na kuwa katika hali mbaya.Mtuhumiwa alipobaini hali hiyo, alimtelekeza na kukimbilia kusikojulikana.

Alidai kuwa baada ya polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa huyo, walikamata vifaa vingi vya tiba zikiwamo dawa za kutibu binadamu.

No comments