Koffi Olomide atimuliwa Kenya kwa kumpiga teke dancer wake (Video)
Mwanamuziki mkongwe wa DRC, Koffi Olomide ametimuliwa nchini Kenya, Ijumaa hii na kurudishwa kwao Kinshasa, baada ya asubuhi ya jana kuonekana akimpiga teke dancer wake wakati akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta, jijini Nairobi.
Olomide alionekana kwenye video akimshambulia mmoja wa dancers wake na kujikuta akibebwa mzobe mzobe jana jioni baada ya kuhojiwa kwenye kituo cha runinga cha Citizen TV.
Staa huyo alikuwa atumbuize Jumamosi hii kwenye viwanja vya Bomas of Kenya.
Hatua hiyo ilikuja baada ya kamanda mkuu wa jeshi la polisi jijini Nairobi Japheth Koome kudai kuwa polisi walikuwa wakifanyia uchunguzi tukio hilo.
Kuna hatihati kuwa Olomide akapigwa marufuku kabisa kukanyaga nchini Kenya.
Post a Comment