Mchekeshaji Kundambanda afariki dunia
Mchekeshaji Ismail Issa Makombe ‘Kundambanda’ amefariki dunia usiku wa kuamkia Ijumaa hii baada ya kusumbuliwa na matatizo ya tumbo kwa muda mrefu.
Mwigizaji huyo ambaye pia aligombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amekutwa na umauti akiwa nyumbani kwao Mtwara.
Akiongea na Bongo5 Ijumaa hii Mwenyekiti wa Chama cha wasanii wa Vichekesho Tanzania, Mkono Wa Mkonole amethitisha kutokea kwa msiba huo.
“Kweli ndugu yetu ametutoka na kwa taarifa zisizo rasmi kesho wanazika, lakini sisi kama wasanii wa vichekesho leo jioni tunakutana na kupanga jinsi ya kuweza kuhudhuria mazishi ya ndugu yetu,” alisema Mkonole.
Katika hatua nyingine wasanii mbalimbali wa filamu pamoja na wanamuziki wameeleza yamoyoni kuhusu msiba huo.
Afande Sele
Kulia sana ni kukufuru, kwa sasa huna hitaji lolote mpiganaji mwenzangu zaidi ya Dua zetu na kukumbuka mazuri yako Mengi.. Siwez kusahau wakati mzuri tuliokua nao ukijaga nyumbani Morogoro. Safari yetu ya Mtwara, kazi yangu ya kwanza ya kisiasa tulienda Mtwara katika kipindi cha Machozi jasho na Damu … Kitambo si kirefu tutakua pamoja tena. Kifo ni safari isiyo na shaka. Umetangulia Ismail.
Kingi Majuto
Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un
Pumzika kwa amani mapembe.
JB
pumzika kwa amani
Post a Comment